Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2018

KANISA LA LAODEKIA

Picha
Kanisa la Laodekia ni kanisa la siku hizi za Mwisho. Ujumbe wa Kanisa la Laodekia unahusu wakristo wa kipindi chetu hasa wa kanisa la  waadventista wasabato. Mimi na wewe tunaweza tukawa ni miongoni mwa wale ambao Yesu amewaongelea katika kanisa la Laodekia. Hivyo kila mmoja na ajitafakari mienendo yake na kama inaendana na tabia ya kanisa la Laodekia inabidi aachane nayo haraka asije akatapikwa kutoka katika kinywa cha Yesu. Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.   Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.  Nakupa shauri...

HISTORIA YA ALAMA YA MSALABA

Picha
Alama ya Msalaba ndio alama kuu sana katika ukristo wa sasa. Karibia makanisa yote ya kikirsto yanaweka misalaba katika makanisa yake. Misalaba pia inawekwa katika biblia mbali mbali katika kasha la kufunikia biblia.  Post hii haizungumzii kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu Msalabani, bali inaongelea ile alama ya msalaba yani Mistari miwili iliyokutana inayoonekana katika makanisa yetu na katika nembo nyingi za madhehebu ya kikristo. Tunajua kuwa alama hii ni maarufu kiasi cha kuwa ikionekana basi inatambulisha ukristo au mtu yoyote anayevaa msalaba basi anaonekana kuwa analindwa na nguvu za Mungu. Kadiri muda unavyoenda watu wanaanza kuabudu alama ya msalaba kiasi cha kufanya sala ikiwa inawekewa alama ya msalaba kama jinsi ilivyo kwa kanisa Katoliki. Watu wengi wa kanisa katoliki wakiwa katika kusali wanafanya ishara ya msalaba. Sasa tuangalie Historia ya alama hii maarufu. Kwa kupitia msaada wa Wanahistoria mbali mbali. Tyrack anasema Ni jambo la kushangaza, na ni ukwe...

144,000 NI NANI?

Picha
Katika Kitabu cha ufunuo wa Yohana Sura ya saba tunaona kuwa kuna watu ambao idadi yake ni 144000 ambao hao ndio washindi wa dhambi kipindi Yesu anakuja tena kwa mara ya pili. Kwa vile watu hawa ambao wamefua mavazi yao na kujiweka tayari na ambao wanatabia ya Kristo katika mienendo yao ya maisha na kweli walioipokea ndio wanayoiishi kabla ya kuja kwake Yesu. Tunajua kuwa Watu hawa 144,000 wanatoka katika wakati huu ambao tuliopo. Katika wakati tuliopo kutakuwa na aina mbili ya waadventista wasabato ambao ni wa Kanisa la Fildefia na wa kanisa la Laodekia. Wa kanisa la Fildefia ndio kanisa la Mungu ambao wanajulikana kama pia ni 144,000 ambao watatiwa Muhuri. Lakini kwa upande mwingine wa kanisa la Laodekia ni waadventista wasabato ambao wanajua ukweli lakini hawaendi sawa sawa na huo ukweli wakijiona kuwa hawana haja na kitu. Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini na nne elfu (Ufunuo 7:4) Tunaona kuwa watu hawa ndio ambao wa...