HISTORIA YA ALAMA YA MSALABA
Alama ya Msalaba ndio alama kuu sana katika ukristo wa sasa. Karibia
makanisa yote ya kikirsto yanaweka misalaba katika makanisa yake. Misalaba pia
inawekwa katika biblia mbali mbali katika kasha la kufunikia biblia. Post hii haizungumzii kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu Msalabani, bali inaongelea ile
alama ya msalaba yani Mistari miwili iliyokutana inayoonekana katika makanisa
yetu na katika nembo nyingi za madhehebu ya kikristo. Tunajua kuwa alama hii ni
maarufu kiasi cha kuwa ikionekana basi inatambulisha ukristo au mtu yoyote
anayevaa msalaba basi anaonekana kuwa analindwa na nguvu za Mungu. Kadiri muda
unavyoenda watu wanaanza kuabudu alama ya msalaba kiasi cha kufanya sala ikiwa
inawekewa alama ya msalaba kama jinsi ilivyo kwa kanisa Katoliki. Watu wengi wa
kanisa katoliki wakiwa katika kusali wanafanya ishara ya msalaba. Sasa
tuangalie Historia ya alama hii maarufu. Kwa kupitia msaada wa Wanahistoria
mbali mbali. Tyrack anasema
Ni jambo la kushangaza, na ni ukweli usioweza kuulizwa, kwamba kabla ya
kuzaliwa kwa Kristo, na tena hata katika sehemu ambazo hazijawahi kuguswa na
mafundisho ya kanisa, alama ya msalaba ilikuwa inatumika kama ni alama
takatifu. Bacchus wa wagiriki, Tyiani Tammuzi, Bel wa wakaldayo, na Norse
Odini, wote walikuwa wanawakilishwa na alama hii ( G.S. Tyack, The Cross in Ritual Architecture and Art,
london 1900)
Inabidi kila mmoja aanze kujiuliza, kwanini alama hii iwe ni alama takatifu
hata kabla ya kuzaliwa kwa Yesu au hata maeneo ambao hawajawahi kusikia habari
za Yesu walikuwa na alama hii? Nukuu hii haijatuambia vyema alama hii ilikuwa
inatumika katika ibada gani. Maana yake ni kwamba kuna uwezekano mkubwa kuwa
alama hii ilikuwepo na ilitumika hata kabla ya ukristo. Lakini tuangalie
mwanahistoria mwingine anasema,
Watu katika maeneo mengi ya Kale walitumia alama ya msalaba katika ibada,
wengine kama vile wamisri waliitumia katika ibada ya Phallusi au ibada ya
kuabudu via vya uzazi wa mwanaume. Ilitumika kama ni ya uzazi. Alama za
misalaba za aina mbali mbali zimekutwa katika kila majengo ya kimisri na katika
makaburi, na inaaminiwa na wengi wenye mamlaka kuwa ni alama ya phallusi
(Ikiwakilisha via vya uzazi vya mwanaume) au ngono. Katika Makaburi ya
wamisri crux ansata (alama ya msalaba yenye duara juu) ilikutwa ikiwa na
Phallusi pembeni (H.Cutner, A
Short History of sex Worship, London 1940 pia angalia The Non christian Cross,
p.183) Mabano wamewekwa na mwandishi
mwenyewe.
Kwa kweli hakuna ambaye atakayesoma hii nukuu bila kushangaa. Ni jambo la
kushtusha kidogo alama ya msalaba kususishwa na ibada za Kipagani tena ni ibada
za kuabudu via vya uzazi wa mwanaume yani uume. Ibada ya kuabudu uume sio ibada
ngeni ilikuwepo katika kipindi cha zamani. Lakini hata leo hii Kuna wajapani
wanaoabudu uume na sikukuu yao inaitwa “Kanamara Matsuri”. Msomaji anaweza
akatafuta katika mtandao. Lakini jambo
la kushitusha ni kwamba alama ya msalaba hii ya leo inayowekwa katika makanisa
na katika biblia mbali mbali kama ndio alama ya ukristo hapo mwanzo kabla ya
ukristo tena katika maeneo ya mbali sana, wamisri walitumia alama hii katika
ibada zao za kuabudu uume. Waliweka alama hii katika majengo yao na katika
makaburi yao na waliitukuza alama hii kama ni alama takatifu. Kwahiyo sasa
tunaanza kuelewa ile nukuu ya mwanzo kuwa ilikuwa inatumika kama alama takatifu
hata kabla ya ukristo, kwasababu ilikuwa inatumika katika kuabudu uume.
Mwanahistoria mwingine anasema
“Ile ambayo sasa inaitwa ni msalaba wa kikristo hapo mwanzo, ilikuwa sio
alama ya kikristo hata kidogo, bali ilikuwa ni tambiko Tau la wakaldayo na la
wamisri. Asili yake halisi ilikuwa ni herufi T ambayo ilikuwa ni jina la Tammuz
kwa kiebrania. Hivyo hivyo katika kaldayo ya kale ilikuwepo katika sarafu zake. (Alexander Hislop, Two Babylon).
Mwana historia huyu anasema wazi kuwa, Alama hii ya msalaba inayotumika
katika makanisa ya kikristo, haikuwa ni alama ya kikristo hata kidogo. Bali
ilikuwa ni alama ambayo inayotumia katika ibada au matambiko ya wakaldayo.
Mpaka hapa kila mwana historia anatoa ushahidi ambao unaonesha kuwa Alama hii
ya msalaba asili yake ni upagani. Kitu cha ajabu ni kwamba kanisa katoliki
linakubali kuwa kanisa la Mitume hawakuwahi kutumia alama hii. New Catholic
Encyclopedia inasema,
“Uwakilishaji wa kifo cha ukombozi cha kristo pale Golgotha haukuwa katika
alama yoyote katika makanisa ya kwanza ya kikristo. Wakristo wa kwanza wakiwa
katika ushawishi wa katazo la agano la kale la kuhusu sanamu za kuchonga,
walikataa hata kuweka kifaa cha mateso ya Bwana”(New Catholic Encyclopedia, 1967)
Pia mwana historia mwingine alisema hivi kuhusu Kanisa la Kwanza la Mitume
“Hakukuwa na matumizi ya alama ya msalaba, na hakukuwa na ukumbusho wowote
wa msalaba”(J.F.Hurst, History
of Christian Church, New York 1897)
Tunaona kuwa Kanisa katoliki linasema kuwa kanisa la Kwanza yani kanisa
ambalo lilianzishwa na mitume hawakuwa na alama yoyote ambayo inawakilisha kifo
cha Yesu pale msalabani. Yani hawakuwa wana misalaba ambayo leo hii inatumika
wala hawakuwa na Alama ya msalaba. Kwa maana kama alama hiyo ya msalaba
ingekuwa ni muhimu sana katika ukristo kama hivi leo, Yesu angewaambia. Lakini
kuna jambo moja tu ambalo Yesu alisema wanafunzi wake wafanye kwa ukumbusho
wake,
Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, [Huu ndio mwili
wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu (Luka 22:19)
Jambo moja tu ambalo Yesu alisema wanafunzi wake wafanye kwa ukumbusho wake
ni kula mkate ambao ni mwili wa Yesu na kunywa divai ambayo ni damu ya Yesu.
Lakini Kristo hakuwahi kuwaambia wanafunzi wake kuwa wawe na alama ya msalaba
kukumbuka alivyotoa uhai kwaajili Yetu. Kwasababu hii ndio maana Kanisa la
Mitume hawakuwa wanatumia alama ya msalaba kama ndio ukumbusho wakifo cha Yesu
bali ukumbusho ambao Yesu aliwaachia ni kula mkate usiochachwa na kunywa divai
pekee. Kwa hiyo alama ya msalaba ni Kitu ambacho sisi wakristo wa leo
tumekifanya kuwa ni ukumbusho wa Yesu lakini hakusema alama ya msalaba iwe ndio
ukumbusho wake. Kitu cha ajabu zaidi ni kwamba alama hii ambayo ilikuwa
inatumika katika ibada za kipagani leo hii ndio inawakilisha kifo cha Yesu. Mpaka
hapa tumejifunza nini
1. Alama ya msalaba ni alama ya kipagani na ilikuwa
inatumika katika ibada za Kipagani za wamisri na wakaldayo
2. Yesu hakutoa ukumbusho wowote ule isipokuwa mkate na
Divai na alisema wazi kuwa huo ndio ukumbusho wake. Kwa hiyo nje ya hiki
alichosema Yesu, sio ukumbusho ambao Yesu anautambua.
Sasa alama ya msalaba katika makanisa ya Kikristo ilianza wapi?
“Sasa
hii alama ya kipagani inayoonekana kwanza ilianza kuingia katika makanisa ya
kikristo huko Misri na kuenea Afrika. Kile alichosema Tertullian katikati ya
karne ya tatu, inaonesha wazi kuwa katika kipindi hicho kanisa la Kathage
lilikuwa tayari limeambukiwa chachu ya kale. Misri ambapo hakukuwa na injili
iliyokuwa imara inaonekana ndio imekuwa kiongozi kuleta alama hii ya upagani.
Aina ya kwanza ya misalaba inayojulikana kama misalaba ya Kikristo iliyokuwa
inaonekana katika Majengo ya Kikristo, ilikuwa ni Tau ya Kipagani au Alama la
uhai ya wa wamisri” ( Alexader Hislop, Two Babylons)
Tunagundua kuwa Alama hii ya kipagani ilianza kuingia katika makanisa ya
Kikristo kuanzia huko Misri. Mitume hawakuwa na alama yoyote iliyokuwa
inakumbusha kifi cha Yesu wala hawakutumia alama yoyote ile. Lakini baada ya
mitume wote wa Mungu kulala usingizi wa Mauti, tunaona kuwa Upagani huu
unaingia katika ukristo na ile alama iliyokuwa inatumika katika ibada za
kipagani sasa imekuwa ndio alama kuu ya imani ya Kikristo. Hivyo kama
tulivyokwisha ona ushahidi wa Kihistoria kuwa Alama ya msalaba ni alama ya
kipagani tunaona kuwa kanisa la waadventista wasabato sasa wameingiza misalaba
katika nembo ya kanisa. Hii inaonesha wazi kuwa Kanisa lipo katika Uvuguvugu na sio moto tena.
Pia wanahistoria wengine wanaamini kuwa Neno msalaba limetokana na neno STRAUROS ambalo lilikuwa na maana mti ulionyooka.
"STRAUROS kimsingi inamaana mti ulionyooka. Na wahalifu walikuwa wanatundikwa ili wafe. Nomino na kitenzi cha neno hili strauroo lina maana mti ambao umenyooka. Na kwaasili inatofautiana na msalaba wenye miti miwili katika kanisa. (W.E.Vine, Expository Dictionary of old and new Testament words 1981)
Kwa maana hiyo inawezekana kuwa Yesu hakusulubiwa katika msalaba ambao leo hii unaonekana bali alisulubiwa katika mti ulionyooka.
Pia wanahistoria wengine wanaamini kuwa Neno msalaba limetokana na neno STRAUROS ambalo lilikuwa na maana mti ulionyooka.
"STRAUROS kimsingi inamaana mti ulionyooka. Na wahalifu walikuwa wanatundikwa ili wafe. Nomino na kitenzi cha neno hili strauroo lina maana mti ambao umenyooka. Na kwaasili inatofautiana na msalaba wenye miti miwili katika kanisa. (W.E.Vine, Expository Dictionary of old and new Testament words 1981)
Kwa maana hiyo inawezekana kuwa Yesu hakusulubiwa katika msalaba ambao leo hii unaonekana bali alisulubiwa katika mti ulionyooka.