Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2018

1YOHANA 5:8 NA MATHAYO 28:19 ZINASEMAJE?

Picha
1.      1YOHANA 5:8 " Kwa maana wako watatu washuhudiao Mbinguni Baba na neno na roho mtakatifu na watatu hawa ni umoja" (1yohana 5:8) Kwa kuanza kabisa, mstari huu ni mstari maarufu sana na unatumiwa kama ndio mstari mkuu unaoonesha kuthibitisha kuwa Mungu ni nafsi tatu. Lakini kwa mtu yoyote yule ambaye ni mwaminifu wa moyo na moyo wake hauna mabishano atajiuliza kwanini katika Mistari mingi ya Biblia Mungu mwenyewe anashuhudia kuwa yeye ni nafsi moja afu mstari mmoja huu ndio ubadili maana nzima ya Mungu mwenyewe? Na kuna watu japokuwa umetoa mistari mingi ya biblia kuonesha kuwa Mungu ni mmoja lakini bado anatumia mstari huu kutokukubali ukweli wa biblia hata kuifumbia macho mistari ya wazi inayoonesha kuwa Mungu ni nafsi moja tu. Sasa taratibu na tuangalie mstari huu kwa kina. Katika mstari huu msomaji na angalie vizuri. Je katika mstari huu wapi panaposema Mungu ni nafsi tatu? Au wapi panaposema kuwa Baba, mwana na Roho ni nafsi tatu za Mungu? Hata we...

MUNGU ANA NAFSI NGAPI?

Picha
Ni wazi kuwa kila mmoja katika kanisa la Adventista wasabato na Wale ambao sio wasabato watajibu swali hili kuwa Mungu ana nafsi Tatu. Hii ni kutokana na Fundisho la Utatu mtakatifu. Nianze kwa eleza nini maana ya fundisho la utatu mtakatifu, Hili ni fundisho linalosema Mungu ni nafsi tatu yani Baba, mwana na Roho mtakatifu. Kwa maana nyingine ni   kwamba Mungu hawezi kuwa na nafsi moja bali siku zote ni tatu.   Lakini Swali la kujiuliza ni kwamba Je biblia Takatifu imesema Mungu ana nafsi tatu? Au ni mapokeo Kutoka katika kanisa Katoliki. Mwanafunzi yoyote mwenye nia ya kweli ya kujifunza pima hichi ninachokisema kama kimetokana na Biblia au hapana, kwa kutambua hilo basi inabidi tuangalie biblia kama jinsi inavyojifunua Yenyewe. Ni muda umefika ambapo inabidi tumwabudu Mungu aliyefunuliwa katika Biblia na sio Mungu aliyetengenezwa na kanisa Katoliki, muda umefika ambapo kanisa la wasabato linabidi liamshwe ili kuzingatia ujumbe wa malaika wa kwanza, ujumbe ambao kanisa ...

ASILI YA FUNDISHO LA UTATU.

Picha
Katika Historia ya ulimwengu fundisho la utatu lilikuwa sio fundisho geni masikioni pa watu. Jamii ya kale ya kigiriki na wamisri na dunia nzima walikuwa na imani ya utatu. Sasa Nianze kwa kutoka nukuu mbali mbali kutoka katika vyanzo vya historia vinavyoheshimika Duniani. Encarta Encyclopedia inasema "Fundisho la Utatu katika teolojia ya kikristo ni fundisho linalosema kuwa Mungu yupo katika nafsi tatu ambazo ni   Baba, Mwana na Roho mtakatifu ambapo nafsi hizi zimeungana na kuwa kitu kimoja. Fundisho hili halifundishwi katika Vitabu vya Agano Jipya ambapo Neno "Mungu" mara zote linamlenga Baba ". (Encarta Encyclopedia) Kila mmoja ni shahidi kuwa Vitabu vya agano jipya Mara zote huwa vinamtaja Baba pekee kuwa yeye ndiye Mungu Msomaji anaweza kujiuliza vipi kuhusu 1yohana 5:8 na Mathayo 28:19, Post hii haitozungumzia ila usikose kusoma Post inayofata lakini msomaji akisoma mistari hio hawezi kuona sehemu inayosema Mungu ni nafsi tatu.  " ...